Nembo ya ZURA
Mamlaka ya ZURA
Ili kufanya haya, ZURA ina Mamlaka yafuatayo:-
Kuanzisha viwango kwa bidhaa na huduma zinazodhibitiwa.
Kuhakikisha kwamba wasambazaji huduma wote wanatoa huduma zinazostahiki.
Kurahisisha na kuzishauri Sekta binafsi kuwa na ushindani mzuri.
Kuhakikisha ushirikiano wa Umma pamoja na huduma za Maji na Nishati kwa jamii kwa kufuata sheria katika shughuli zao.
Kupokea, kukabili na kutatua malalamiko ya Watumiaji wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar.
Kurahisisha utatuzi wa malalamiko na migogoro ya Wateja.
Kulinda na kutunza Mazingira, Rasilimali asilia na Afya na Usalama wa Watumiaji.
Mafanikio
Katika Kipindi cha Miaka Mitano (5) ZURA imepata mafanikio yafuatayo kwa ujumla:-
Ujenzi wa Jengo jipya la Ofisi za ZURA
Maandalizia ya Mradi wa Bohari na Bandari ya Mafuta na Gesi Bumbini/Mangapwani.
Ujenzi wa Nyumba za Wanakijiji cha Dundua kupisha Mradi wa Bohari na Bandari ya Mafuta na Gesi Bumbwini/Mangapwani.
Katika Kipindi cha Miaka Mitano (5) ZURA imepata mafanikio yafuatayo katika sekta ya Mafuta:-
Kuandaa Kanuni za kudhibiti sekta ya Mafuta.
Kutoa bei elekezi za Mafuta kila mwezi.
Kuweka fomula ya uwazi katika ukokotoaji wa bei za mafuta.
Kuhakikisha mafuta yanayoingia nchini yapo katika kiwango bora.
Kuhakikisha vipimo vya mashine za kuuzia mafuta viko sahihi.
Kutoa miongozo ya kuboresha vituo vya Mafuta.
Kutoa leseni kwa wawekezaji katika sekta ya Mafuta.
Kufanya ukaguzi mara kwa mara katika vituo na bohari za Mafuta.
Katika Kipindi cha Miaka Mitano (5) ZURA imepata mafanikio yafuatayo katika sekta ya Gesi (LPG):-
Kuandaa Kanuni za kudhibiti sekta ya Gesi (LPG).
Kuandaa Mikutano na Wadau wa sekta ya Gesi (LPG).
Kutoa Elimu kwa Wauzaji na Watumiaji wa Gesi (LPG).
Katika Kipindi cha Miaka Mitano (5) ZURA imepata mafanikio yafuatayo katika sekta ya Umeme:-
Kuandaa Kanuni za kudhibiti sekta ya Umeme.
Kuandaa Mikutano na Wadau kujadili Gharama ya Huduma ya usambazaji wa umeme Zanzibar (Cost of service study).
Kutoa Elimu kwa Wauzaji na Watumiaji wa Umeme.
Katika Kipindi cha Miaka Mitano (5) ZURA imepata mafanikio yafuatayo katika sekta ya Maji:-
Kupatikana kwa Mshauri Elekezi katika Sekta ya Maji (Consultant).
Kuisaidia ZAWA kununua Mita za Maji.
Kutoa Elimu kwa Wauzaji na Watumiaji wa Maji.
Changamoto
ZURA katika utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku inakutana na changamoto zifuatazo:-
Kutokutoa au kuchukua risiti kwa wauzaji na wanunuzi wa nishati ya mafuta.
Uelewa mdogo juu ya majukumu ya ZURA kwa Taasisi zinazodhibitiwa na jamii kwa ujumla.
ZURA itaanza rasmi kudhibiti sekta ya Umeme na Maji.
Mikakati
ZURA imeandaa Mpango Mkakati wa miaka mitano (2017-2022). Mpango huo uliandaliwa kufuatia mchakato kamili ambao ulijumuisha wadau, Sheria ya ZURA na nyaraka nyengine muhimu za upangaji Mipango ya kitaifa kama vile Dira ya 2020, MKUZA na Manifesto ya Uchaguzi wa Chama cha Mapinduzi (CCM).
ZURA katika kukabiliana na changamoto zilizopo imejipanga kufanya yafuatayo.
Kuongeza kasi ya kujitangaza zaidi ili jamii iweze kuelewa majukumu na uwezo wa ZURA.
Kuongeza ushirikiano na wadau wa sekta za inazosimamia.
Kutayarisha Kanuni na hati nyengine za kisheria ili kusimamia sekta ya Umeme na Maji.
Kufanya Ukaguzi wa mara kwa mara kwenye Vituo na Bohari za Mafuta.
Kuanzisha mfumo wa kuweka alama katika bidhaa za Mafuta.